Hisapepe Kituo Cha Msaada - Maswali Ya Mara Kwa Mara ya Wanachama Uk. 2
Ukurasa wa Pili wa Maswali ya Mara Kwa mara
|
-
- Kiteknolojia ndiyo inawezekana ila kimantiki hatuoni sababu. Huduma hii hatujaiwezesha maana njia ya malipo uliyochagua inakuwezesha kuhamisha salio tunashauri utumie hiyo. Tunataka kuwalipa wanaHisapepe.com halisi pekee.
-
- Hisapepe inaweza kukulipa mara tu ufikiapo kiwango cha kulipwa, lakini kwa sasa tumependelea uombe kulipwa pale unapohitaji. Huwezi kupokea malipo hadi utakapoomba, vilevile kama njia unayotaka kilipwa nayo ina gharama za kuhamisha hii itamaanisha Tsh 1000/- haiwezi kutumwa maana wanakukata gharama za utumaji hivyo salio lako linatakiwa kuwa Tsh 1000+gharama zao. Sababu nyingine hupokei malipo huenda ni kwamba umekiuka masharti ya huduma hii, tunakushauri uwasiliane na huduma/msaada kwa mteja.
-
- Sababu kadhaa. Tangazo limeshapita muda wake kwa kuwa limesetiwa liangaliwa kabla ya tarehe unayolisoma wewe. Au tangazo linalipia idadi za kufunguliwa (hits/clicks) na sasa idadi yake imeshatimia kwaio limekwisha muda wake. Au umeshafungua tangazo hilo na sasa ni kama unafungua tena, mtambo wetu hautakupa pesa kwa ujanja huu hata ukitumia kompyuta nyingine. Tangazo lolote linalofikia muda/idadi ya kufunguliwa kuisha halitampatia mwanachama pesa. Jitahidi uwe unasoma matangazo kabla hayajakaa sana, hata hivyo hii ni mara chache sana itakutokea.
-
- Njia kadhaa zipo, unaweza kuweka anuani yako ya mwaliko katika tovuti yako au blog yako, au ukurasa wako wa mitandao mingine kama inaruhusu, watakaovutiwa na kujiunga watakuwa ni waalikwa wako. Unaweza kuweka anuani yako ya mwaliko kama saini (signature) au barua pepe zako (nenda options ndenda signature kwa yahoo, gmail, hotmail n.k). Unaweza pia kuchapisha vipeperushi, sms au namna yoyote ya kutaarifu isipokuwa SPAM (kutuma kwa usiowajua). Kuna njia nyingine zimeorodheshwa ndani katika akaunti yako ya Hisapepe, ingia kisha nenda “Lipwa Kualika” ujionee njia zilizopo
-
- Anuani hii inapatikana katika kitengo mahsusi cha mialiko ya hisapepe.com. Ingia katika akaunti yako kish utaona ”Lipwa Kualika” (katikati chini) na “Alika Marafiki” (kushoto pembeni) huko utaona anuani yako ya mwaliko. Mara nyingi kama umejiunga kama MrSampuli anuani yako itakuwa http://www.hisapepe.com/pages/index.php?refid=MrSampuli au kama ni umejiunga kama anifa basi anuani yako ya mialiko ni http://www.hisapepe.com/pages/index.php?refid=anifa wote watakaoibofya hii na kuja hisapepe.com na kujiunga watakuwa wanakupatia salio kwa matangazo watakayoona. Maelezo mengine kuhusu ya mabango n.k utayapata ukiingia katika anuani yako katika ”Lipwa Kualika” .
-
- Utapata 8% ya kile anachopata uliyemwalika, na 2% ya kile wanachopata walioalikwa na uliyemwalika. Pia Kwa sasa kwa kuanzia tunatoa Tsh 50 kwa kila nayejiunga kwa mwaliko wako mpaka ofa hii itakapoisha.
-
- Ndiyo, mapato yako kutokana na uliowaaalika hukusanywa mara moja katika kila masaa 24 na kuwekwa katika akaunti yako. Unatakiwa kuwa mwanchama hai walau kwa 25% ya uhai wao ili upate malipo toka kwa uliowaalika.Pia usikae sana bila kuja hisapepe.com na kuingia ili akaunti yako isionekane mfu)
.
-
- Unakaribishwa. Ingia katika akaunti yako kisha nenda "Tumia Pesa yako" katika menyu za kushoto, changua matangazo utakayo kununua na anza kampeni yako, utalipia kwa salio lako. Kama unataka kutangaza kama watangazaji wengine unalazimika kufungua akaunti ya utangazaji au unanaweza kuwasiliana nasi.
-
- Ni Utaratibu wa kuwajibika kwa jamii. Katika ulimwengu huu wa ushindani wa biashara, kukamia kutangaza tu si dawa. Hisapepe inawakumbusha wafanyabiashara wajiwajibishe kijamii, waisaidie jamii. Kivipi? Fikiria mfano janga la ukimwi, watu wanateketea. Wanaweza kuiokoa jamii kwa kutuma ujumbe mahsusi wa UKIMWI kwa watumia internet, hii ina manufaa kwao kwani ujumbe unaotumwa utasema “Umeletwa kwako na hao watangazaji au Bidhaa yako” ni sehemu ya wajibu kwa jamii. Ila ni sehemu ya mahusiano kwa umma pia (Public Relations) Okoa Kiazi hiki! Tumia Intenet Kiuwajibikaji!
-
- Hisapepe.com ni zao la Kampuni ya Hisapepe. Ni Kampuni ya nyumbani Taznania na ipo kwa ajili yako. .
-
- Ni kampuni ya kimasoko ila inalalia zaidi upande wa masoko kwa njia ya motisha (INCENTIVE BASES MARKETING). Kama kampuni nyingine usajili hufanyika kwa mamlaka husika iliyoteuliwa na serikali ya Tanzania yani brela
-
- Lengo letu kuu ni kuanza kujenga tamaduni ya biashara mtandaoni yani bila watu kuonana. Habari ya mama kutembea kilomota mia kupeleka ada ya mtoto ni enzi zilizopitwa. Hatuoni sababu yawe kuja kwetu, wewe mteja ama mtangazaji maana kila kitu unakipata ukiwa kwako. Inapotokea una ulazima kutuona kwa mambo mengine unakatibishwa sana.
-
- Wanachama wetu wana jibu la swali hili. Utapeli ni pale unapotakiwa utoe kitu na baadaye unajikuta unapewa kidogo kuliko ulichotoa ama unakosa chote, sisi hatuchukui chochote toka kwa mwanachama wetu, kujiunga ni hiyari na kujitoa ni hiyari. Tunachofanya ni kukupa nafasi ya kujiongezea kipato. Sisi hatutoe malipo, tunasimamia malipo toka kwa watangazaji, sisi ni kama wakala wa kuhakikisha haki kati ya wanachama na mtangazaji. Mialiko tunayotoa pesa ni gharama zetu za kukuza mtaji wetu maana mtaji wetu sisi ni wanachama. Mwanachama anapoalika halipwi kutoka kwa pato la mwanachama aliyealikwa bali toka mfuko wetu hisapepe, si upatu.
- Tembelea www.hisapepe.com/pages/swahili/contact.php kama una swali ungependa kumuuliza muhudumu moja kwa moja. Kama hayupo acha ujumbe
|
| Rudi Juu | Ukurasa wa nyuma wa Maswali |
|