|
hisapepe.com
HAYA NI MAELEZO TOSHA JUU YA HISAPEPE.COM
Msaada wa jinsi ya kutumia hisapepe
Kabla ya yote zingatia
Masharti yetu na ilani ya faragha
Soma Maswali ya mara kwa mara
Kuchagua lugha unabofya bendera za mbele
Huruhusiwi akaunti mbili
TUANZE SOMO LETU:
(unaweza kubofya kichwa cha habari na maelezo yatapanda hapa juu)
Hisapepe ni nini
- Menyu za nje za hisapepe
- Maskani
- Jiunge
- Eneo La Mwanachama
- Tangaza
- Vitangazo
- Kuhusu sisi
- Msaada
- Takwimu
- Kuchagua Lugha
- Jinsi ya kujiunga
- Jinsi ya Kuingia
- Menu za ndani za hisapepe
- Wasifu wako
- Salio Lako
- Pesa ulizowahi kupata
- Uliowaalika
- Matangazo yako
- Uanachama VIP
- Pata Pesa
- Inbox
- Lipwa kubofywa
- Vijitangazo
- Lipwa kutafiti
- Lipwa kusafu
- Lipwa kujiunga
- Lipwa Kupitia
- Lipwa kuchati
- Lipwa kualika
- Alika Marafiki
- Tumia Salio Lako
- MAtangazo Maalumu
- Chukua pesa yako
- Mijadala
- Waliolipwa
- Bab’ Kubwa
- Wanachama Aibu
- Ujumbe toka utawala
- Habari za Mwanachama
- Ujumbe toka hisapepe
- Toka Nje
Hisapepe ni nini?
Hisapepe ni tovuti inayolipa wanachama wake kwa kile wanachokifanya katika tovuti hii. Hisapepe ni kwa ajili ya matangazo, utafiti na uelimishaji. Tovuti hii ni ya kipekee maana imejtolea kugawana mapato na wanachama wake. Matangazo, tafiti, uelimishaji ama ujumbe unaolipiwa kupitia hisapepe utawafikia wanachama na kuwanufaisha kwa pesa kadiri ya gharama zilizotozwa na hisapepe, kila mshiriki atajipatia sehemu ya malipo hayo yaliyotolewa na mwenye tangazo.
Hebu tuangalie mfano huu: Kampuni ya Sabuni inataka kutangaza kuwa imekuja na sabuni mpya inaitwa “Nawiri”. Inataka tangazo hili liwafikie watu 10000. Kampuni ya Hisapepe inakubaliana na Kampuni ya Nawiri kuwa tangazo hilo la sabuni litatumwa kwa gharama ya Tsh 1,000,000/= (kwa mfano tu). Kampuni hii ya sabuni inakubali na kulipa (italipa pia ada ya ziada ya tangazo lake mfano Tsh 5,000/=).Sisi Kampuni ya Hisapepe kupitia mtambo wa hisapepe.com tunatuma barua pepe kwa wanachama 10000 zenye tangazo hili, kwa hiyo Tsh 1,000,000/= ukigawanya kwa wanachama 10000 ina maana kila anayesoma email hiyo hapo hapo anajipatia Tsh 100/=. Hivi ndivyo kimsingi unavyopata pesa ukijiunga hisapepe.com. Kukiwa na matangazo kumi au hii kampuni ikitaka tangazo hilo lijirudie mara 10 basi utapata Tsh 100x10=1,000/=. Ndivyo rahisi namna hii unajipatia Tsh 1000 yako kwa kusoma tu email ya matangazo. Kila kitu kipo wazi, ni dhahiri hisapepe.com inajipatia Tsh 5000 yani ule mfano wa ada ya ziada. Ni utaratibu mzuri kwa maana kila mtu anafaidika, sisi, mwanachama na Kampuni hiyo ya sabuni (au kampuni yoyote itayopenda kutangaza)
Hisapepe.com ina teknolojia ya kisasa kabisa tena ni ya hali ya juu. Kila baruapepe unayotumiwa ina lebo ya kipekee “unique link & code” ambayo itathibitisha umeisoma na hapo hapo akaunti yako itaongezewa salio kadiri ya bei ya tangazo hilo. Huwezi kudanganya kwa kuifuta au kutoifungua barua pepe hiyo, unapata pesa kwa kusoma tangazo!
Ukishajikusanyia pesa yako basi unaweza kuomba kulpwa yan kudroo (withdraw) pesa yako. Pesa hii unaweza kuipokea kama muda wa maongezi wa simu yako yani airtime ama pesa taslimu. Kama mjasiriamali unaruhusiwa pia kutumia salio lako kulipia huduma kadhaa, kwa sasa ni kulipia huduma ya kutangaza biashara/ujumbe wako. JIONGEZEE KIPATO SASA!
Menyu za nje za Hisapepe
Hizi ni menyu zinazoonekana ukiwa nje yaani kabla ya kutumia jina lako na neon la siri na kuingia ndani ya hisapepe
Maskani
Huu ni ukurasa mkuu wa mwanzo, mara nyingi utatua hapa ukija hisapepe.com hapa mbele kuna matangazo makubwa juu na nchini na pia kuna taarifa za mwanachama na mtangazaji juu ya faida na ofa za hisapepe. Pia hapa unaweza kuingia na ni sehemu hii tu kulia ina eneo la wewe kuingia hisapepe. Matangazo haya ya mbele hayatakulipa. Ukibonyeza Bendera ya Tanzania utabadili hisapepe.com yote na kuwa Kiswahili. Ukibonyeza ya ya Marekani utapata hisapepe.com ya kiingereza.
Jiunge
Hapa ni sehemu yako kujiunga na kuwa mwanchama wa hisapepe. Jinsi ya kujiunga ni rahisi. Bonyeza JIUNGE kisha utaombwa uigize anauani yako ya barua pepe yaani mfano maikomtabejr@yahoo.com kisha bofya Jiunge. Hisapepe.com hapo hapo itakutumia barua pepe (email) ya mwaliko katika anuani hiyo uliyoingiza. Ujumbe huo una anuani ama link ya kubofya. Utachagua kama unataka kujiunga kwa Kiingereza ama Kiswahili. Bonyeza anuani/link hiyo kadiri ya lugha upendayo na utaletewa fomu ya kujiunga hisapepe.com. Fomu ya kujiunga inataka. NB: Kama hujapokea ujumbe huu basi umepelekwa katika folda la SPAM, JUNK ama BULK angalia huko kisha uondoe kwa kusema “Mark as Safe” ama “Not SPAM” kufanya hivi kutafanya ujumbe wowote (na matangazo) toka hisapepe.com kuja kwako na si kutupwa spam/junk/bulk folda. Njia nyingine rahisi ni kuhifadhi anauni za hisapepe.com katika orodha yako (addressbook) haswa support@hisapepe.com ambayo ndio inatuma mawasiliano na rewards@hisapepe.com ambayo inatuma matangazo
Username/Jina la Kuigilia.
Tunga jina lako utalolitumia hisapepe.com, jina hili ndio litakuwa lako hapa hisapepe.com. Hutaweza kulibadili na litaonekana na wanachama pale tu utapochat nao na kama utashiriki mijadala amakuorodheshwa katika orodha ya waliolipwa (ukipenda)
Vingine ni Anuani, Nchi, Mkoa, Namba ya simu (iwe sahihi)
Pia unahitaji kuiambia hisapepe ungependa matangazo ya namna gain, chagua hapa aina ya matangazo unayotaka kutumiwa.
Chini ni vigezo vya kushiriki tafiti mbalimbali. Kumbuka hakuna anayeona fomu hii kwa hiyo kuwa huru kujielezea, kudanganya ni kujidanganya maana hisapepe.com itakuletea matangazo au tafiti zisizoendana nawe ama utarukwa kama kuna tafiti na hukuelezea vigezo vyako. Usisahau kuwa unatakiwa kuchagua njia ya malipo kati ya zilizoorodheshwa hapo. Pia tunga neon lako la siri yaani password na hivyo utaingia hisapepe kwa neno lako la siri pamoja na jina la kuingilia ama anuani ya barua pepe.
Eneo La Mwanachama
Hii ni sehemu yako mwanachama na unatakiwa kuingia kuweza kuona vilivyomo hapa. Pia muda wowote ukibofya hapa utarudi ukurasa mkuu wa ndani ya hisapepe. Pia kila baada ya kufanya kitu na ukajikuta hauko menyu kuu basi bonyeza hii na utarudishwa sehemu ile uliyotua ulipoingia ambapo kushoto ni menyu zote na kati ni menyu kuu za kushiriki kupata pesa.
Tangaza
Kwa wale walio watangazaji, wadhamini, walimishaji, makampuni mashirika na hata wajasiriamali wanaotaka kuufikia umma wa hisapepe hapan ndipo pa kuanzia. Ukibofya Tangaza utapata kufahamu bei zetu na aina ya matangazo tunayotoa. Kama wewe ni mwanachama huna haja yah ii, ukiwa ndani hii ipo na inapatikana katika sehemu ya faidi salio lako. NB:Ukurasa wa tangaza upo kiingereza, si teknolojia bali ni sababu za kibiashara zaidi. Ukitatizwa waweza kutuandikia advertising @ hisapepe.com
Vitangazo
Hivi ni vitangazo vidogovidogo huwa kizungu vinaitwa Classifieds. Tumeviweka hapa nje ili kuwafikia walio na wasio wanachama. Kama ni mwanachama unatakiwa kwanza kuingia ndani ili uweze kujipatia pesa ukivisoma.
Kuhusu sisi
Ni Wasifu wa Hisapepe.com
Msaada
Kila ukikwama tafadhali njoo hapa kwanza upate kusaidiwa. Kuna mhudumu aliye tayari kuzungumza nawe. Kama hayupo unaweza kuacha ujumbe, pia chini kuna sehemu ya “Wasiliana nasi” ambapo unaweza kupata msaada. Kuna namba ya simu pia kama unahitaji na pia tunajitahidi. Jisikie huru tupo kukufanya ujisikie nyumbani.
Takwimu
Kila ajiungae anasema anapendelea nini, orodha ya wanachopendelea inapatikana hapa kwa ajili ya watangazaji. Pia tunaweka idadi ya matangazo, wanachama na kiasi cha pesa hisapepe imeshakipeleka kwa wanachama wake.
Kuchagua Lugha
Bofya bendera ya Tanzania kuchagua Kiswahili, Ya Marekani kuchagua kiingereza (tumetumia zaidi kiingereza cha kimarekani)
Jinsi ya Kuingia
Katika ukurasa wa maskani kuna sehemu ya kuingia mwanachama, sehemu hii inahitaji jina la kuingilia ama anuani ya barua pepe, ulipojiunga uliotunga jina lako la kutumia hisapepe yaani username, hapa linatakiwa likiambatanishwa na neno lako la siri (password) kisha utaweza kuingia. Bofya INGIA uweze kuingia
Menu za ndani za hisapepe
Wasifu wako
hii ni ile fomu uliyojaza ulipojiunga, unaweza kuabadili taarifa zako binafsi kadiri ubadilikayo, kwa mfano ukinunua gar ungependa kutangaziwa mambo ya magari, unaweza kuja kubadili hapa. Ukitaka kubadili neno la siri (password) pia unaweza. Kila kitu unaweza kubadili isipokuwa jina lako la kuingilia (username)
Salio Lako
Kila ufanyapo ‘kazi’ hapa hisapepe.com unapata haki yako, pesa hiyo hukaa hapa kama salio. Kisha siku ukipenda unaweza kuchukua pesa yako.
Pesa ulizowahi kupata
Hii ni historia ya mapato namatumizi yako ya hisapepe. Kama ulipata Tsh 10000, ukatoa tsh 2000, ukanunua tangazo la tsh 4000 basi vyote vinaonekana hapa mpaka saa na sekunde uliyofanya huo mwamala. (bank statement yako hii)
Uliowaalika
Ni haki yako kufahamu watu uliowaalika ambao unapata kamisheni yako toka kwao kila wanaposhiriki na kupata kazi hisapepe. NB: hawa si uliowaalika wote, hawa ni uliowaalika wakajiunga, hatuoneshi wala kurekodi umemwalika nani na nani, tunarekodi anayekuja kwa mwaliko wako tu. Na pia Ukimwalika Maria kumbe amealikwa na Joseph pia, akija kwa mwaliko wa Joseph ataonekana kwa Joseph na si kwenu wawili ama kwako. Inaangalia Maria alitumia mwaliko wa nani kuja kujiunga hisapepe na si nani alimwalika kwanza.
Thibitisha Umelipa
Hii ni sehemu ya kuthibitisha umelipia tangazo (kwa wale wanaotangaza tu)
Matangazo yako
Kama umewahi kutangaza hisapepe basi takwimu za matangazo yako zinapatikana hapa. Hii inakupa kila kitu kuhusu mafanikio na ufikio (coverage/clicks) ya matangazo yako. Takwimu hizi ni muhimu kuthibitisha haki yako ya msingi kama mtangazaji unastahil kuona pesa yako imekwenda kihalali.
Uanachama VIP
Huduma hii itakujia baadaye. Twende kwanza na hizi kadhaa, wataalamu wa masoko wanaamini kitu kikianza kiwa cha kawaida na kisiwe kigumu, haya mengine tumeyazuia mpaka wote tutapokuwa tumeifahamu hisapepe kinagaubaga.
Pata Pesa
Kama kuna menyu kuu basi hii ndiyo yenyewe. Kuirahisisha zaidi imepewa kurasa nzima ya eneo la mwanacham na hapo utaona kuna njia za kupata pesa zilizopo hisapepe.
- Inbox
- Lipwa kubofywa
- Vijitangazo
- Lipwa kutafiti
- Lipwa kusafu
- Lipwa kujiunga
- Lipwa Kupitia
- Lipwa kuchati
- Lipwa kualika
Alika Marafiki
Ni njia ya ziada ya kualika marafiki
Tumia Salio Lako
Hapa ni sehemu ambayo inakuruhusu kutumia ulichovuna hisapepe. Una njia tatu za kutumia pesa yako, kuitumia kutangaza hisapepe, kupata matangazo maalumu na mwisho ni KUICHUKUA PESA YAKO
Matangazo Maalumu
Haijaanza kwa sasa, itakujia punde
Chukua pesa yako
Ni sehemu ya kuchukua pesa yako yani kudroo (withdrawing). Sehemu hii inahitaji kwanza Uwe umefikia kiwango kinachoruhusiwa kutoa. Kwa sasa hisapepe.com imeweka kiwango kidogo kabisa yaani Tsh 1000/=. Salio lako likiwa Tsh 1000 au zaidi basi sehemu hii itakuwa inafanya kazi na utapata kitufe cha “Withdraw” ili uweze kutoa pesa yako. Kabla ya hapo hapataonesha kitufe hicho. Lazima uoneshe njia ya malipo unayoitaka, lazima uoneshe ni kiasi gani unataka, kama hutaki kubakiza kitu unataka yote basi tia alama ya vema kisanduku cha “Full Balance”. Hakikisha pia unaingiza akaunti ambayo tutakutumia pesa yako kama ni simu basi weka namba itakayopokea malipo. NB: Chini unaulizwa kama ungependa kuorodheshwa katika orodha ya waliolpwa, toa alama ya vema kama hupendi kutajwa umelipwa (hatuoneshi undani zaidi ya jina lako la kuingilia (username) nakiasi, taarifa zako kamwe hazionekani na mwanachama mwingine kwa namna yoyote ile.
Mijadala- Kwa kuwa tunazingatia la kwanza ni uhalali na haki ya kila mmoja katika kupata malipo, la pili ni kuhakikisha mtu hanuni wala kuumizwa. Tanzania ina blogs nyingi na tovuti nyingi sana, hatutaweza kwenda kujibu lalamiko au hoja ya kila mwanachama na asiye mwanachama huko. Kwa kuzingatia hilo tumeiona ni heri kukawa na sehemu ya wanachama kuijadili hisapepe. Unaruhusiwa kusifia, kulalamika, kuponda na kusema lolote kuhusu hisapepe katika mjadala huu. Timu ya hisapepe.com itajitahidi iwezavyo kujadili kila hoja na kufikia muafaka. Huna haja kujinga na Ukumbi huu wa mjadala, ukishakuwa mwanachama hisapepe tayari unaunganishwa na huku. Kumbuka ia mjadla huu ni sehemu ya hisapepe.com kwahiyo ukibofya kutoka nje (sign out) inakusaidia kufanga pia akaunti yako hapa hisapepe.com
Waliolipwa
Hawa ni baadhi ya wale waliokubali kuidhihirishia ulimwengu ya kuwa hisapepe.com inalipa na si mchezo wa kuigiza.
Bab’ Kubwa
Hawa ni wanachama ambao kwa vigezo ilivyotajwa hisapepe.com imewaona kama ni mfano wa kuigwa.
Wanachama Aibu
Hawa kwa sababu moja au nyingine wameshidwa kutimiza masharti ya hisapepe na wanaonekana ni wanachama wa kutuaibisha, sababu Kubwa ni udanganyifu na kujaribu kuwa na akaunti nyingi za hisapepe, huo ni wizi!
Ujumbe toka utawala
Kuna wakati tutalazimika kutumia ujumbe wa shuruti kwa maana ya kwamba ujumbe huu LAZIMA uujibu ili uendelee kushiriki na kupata pesa, mfano umekamatwa mdanganyifu mfumo wa hisapepe.com unaweza kukulazimu ukiri hutarudia kosa, usipojibu hutapokea tangazo kamwe.
Habari za Mwanachama-Kama kuna taarifa mpya za hisapepe tutaambiana hapa ama katika barua pepe yako.
Ujumbe toka hisapepe
Huu una tofauti kidogo, huwa ni mazungumzo kati yako na hisapepe.com, ikitokea una ka kambiwa binafsi na si wanachama wote unaupata hapa, ujumbe huu unaweza kuujibu kama tu unavyojimbu barua pepe ama sms
Toka Nje
sehemu ya kufunga eneo lako la hisapepe mara baada ya kufanya kazi. KUMBUKA, KUTOFUNGA SANDUKU LAKO HISAPEPE UNAWEZA KUIBIWA KAMA MWINGINE AKILIKUTA WAZI NA KUCHUKUA PESA YAKO. HISAPEPE HAITAHUSIKA NA HILI. TUNAJITAHIDI KUKUFAHAMISHA KWA BARUA PEPE KILA UTOAPO PESA, kama si wewe ni here ukaripoti mapema support @ hisapepe.com
NJIA ZA KUPATA PESA HISAPEPE.COM
Njia hizo ni:
Inbox:
Unalipwa kwa kusoma email za maangazo. Unaamua Email hizi zikae hapa hisapepe ama pia zije kwenye sanduku lako la email yani huko yahoo, hotmail, gmail n.k. Unalipwa kwa kila email utakayopokea. JINSI YA KUSHIRIKI: Nenda hisapepe.com, ingia, kisha katika Menyu kuu za kati Bofya “Inbox” Ndani utaona barua pepe ambazo ni vichwa tu. Bofya kichwa na dirisha jipya litafunguka na katika barua pepe hiyo kuna PAID LINKS ama anuani ambayo itakupatia pesa, bofya anuani hii kishwa utafunguliwa tangazo lililo ndani yake. Kumbuka tangazo hili lina muda kwa juu ambao LAZIMA MUDA HUU UPITE TANGAZO HILO LIKIWA WAZI ili uweze kujipatia pesa. Kama ukijaribu kufunga baso akaunti yako haitaongezwa. Kama umeletewa barua pepe katika email client yako yani yahoo, gmail, hotmail, outlook nk bofya PAID LINKS ambazo ni anuani za malipo kisha utarudishwa hisapepe.com sehemu ya kuingilia, ingiza jina na neno la siri kisha litakuja tangazo lililotumwa na saa ya juu inahesabu mua na hatimaye utapatiwa pesa yako. USIJARIBU KUFUNGA TANGAZO KABLA HUJAAMBIWA AKAUNTI YAKO IMEONGEZWA, usipotii unajikosesha pesa na unapoteza muda. Ya kuzingatia, barua pepe za sanduku lako katika hisapepe zitafutwa kila baada ya siku 31 (mwezi), pia zingatia kila tangazo utumiwalo lina muda wake usishangae kukutana na tangazo limeshaisha muda (limeeksipaya). Mantiki ni kwamba kama ni tangazo la mechi ya Tar 23, wewe ukilisoma tar 24 huwezi kupata pesa, mechi imepita! KUWA MAKINI, chini kabisa ya kila barua pepe tunaweka onyo la “Usiguse anuani hizi” “Shouldn’t touch these links” ukijaribu kuzibofya akaunti yako itatozwa pesa na salio litapungua. Hizi zimewekwa kuikinga hisapepe na wataalamu wa kompyuta ambao wanaweza kutengeneza program (BOTS) na kuingia kubofya links bila wao kuhiiki na kisha kujipatia salio, BOTS si mtu, zitapitliza na hapo watajikuta wanapoteza wao)
Lipwa Kubofya
Haya ni mabango (banners) ambayo yapo sehemu hii, ukiyabofya yanafunguka na kukupeleka katika ukurasa wa tangazo ili ulisome, unapata pesa kila ufunguapo tangazo la kubofya. Tangazo hili lina muda unaotakiwa kuwepo hapo, ni sekunde kadhaa, muda huo unahesabiwa na saa ya Hisapepe, ukitimia salio lako linaongezwa pesa hapo hapo. Mtindo ni ule ule, tunataka mtangazaji naye apate haki yake, ukijaribu kufungua tangazo na kulifunga kabla ya muda wake kuisha basi hutapata kitu. Kujaribu kufungua matangazo mengi kwa pamoja ni kujidanganya hutapata kitu.
Vijitangazo
Hivi ni vijitangazo vidogodogo (Classifieds) ambavyo vitakuingizia pesa pia, pia vinaonekana kwa wanachama na wasio wanachama, ni hivi tu na yale ya nje ya tovuti yanaonekana kwa wasio wanachama, walio wanachama wanalipwa kwa kuvisoma, wasio wanachama wanajipatia taarifa bila malipo. Bofya aina ya tangazo inayoonesha kuna matangazo mangapi (e.g 3 ads au 5ads) yani matangazo matatu ama matano kutegemea na yaliyopo, chini kuna sehemu mbili (member click here) na (visitor click here) wewe utabofya member click here na utajipatia pesa. Lazima uingie kwanza hisapepe uweze kulipwa.
Lipwa Kutafiti
Hii ni kwamba yapo mashirika yanayoendesha tafiti (risachi/saveizi) na kuhangaika mtaani kuhoji watu, hii ni mwisho, hapa utapata dodoso (questionnaires) na utashiriki mahojiano mbalimbali na kwa kufanya hivyo Hisapepe itakulipa pesa nzuri tu kutegemeana na urefu na ugumu wa hojaji/tafiti/savei/kweshenea. Mara nyingi hii ni kama fomu tu na unajibu maswali na kumaliza na kujipatia pesa yako nzuri tu. Ripoti tunayoipeleka kwa mtafiti huyo aliytupa dodoso haitakuwa na taarifa zako zozote, jisiki huru hisapepe.com haitajua nani amejibu nini maana hatuambatanishi majibu na mapato.
Lipwa kusafu
Hii ni namna nyingine ya kukupa pesa, yani matangazo ya kusafu (ni kama mtiririko wa slideshows ya powerpoint) yanakuwa yanapita nawe unayatazama kimtiririko, unayatazama kama TV. Kwa kila tangazo uangalialo unajipatia pesa na kwa kila tangazo uwekalo unalipia pesa hii ni nafasi ya ujasiriamali, ila usijali pia maana kuna YA BURE KABISA ili kukuza ujasiriamali Tanzania, tangaza biashara yako hapa BURE! Unapobofya Lipwa kusafu unakutana na orodha ya lipwa kusafu #1, #2, #3,#4, kila moja ina bei tofauti, ya kwanza ina bei ya juu zaidi (unalipwa pesa kubwa kwa kila tangazo, ya pili inapungua kidogo, ta tatu na hatimaye ya nne ambayo ni “BURE”. (kitekonolojia kulilazimika kuwa na kitu kuepuka infinity yano namba gawanya kwa sifuri ndio maana ripoti itonesha 0.000001TSh ambayo ni Bure, yani utahitaji kuweka matangazo milioni moja ukatwe Tsh 1. Anuani uionayo hapo juu ni yako, ukiibofya basi yataanza kutiririka na kumbuka kila baada ya muda fulani pale juu kakika saa utaombwa kuingiza neno ulionalo, hii ni ulinzi kuepuka BOTS (program zinazojiendesha ) na pili kuepuka mtu kuacha mtiririko kumbe hayupo. Kama mtiririko ni mrefu sana na wewe umetosheka basi bofya “SAVE and EXIT” ili ihifadhi na kuondoka na kukupatia pesa yako. Usijaribu kufunga ama kuMINIMIZE dirisha hilo hutapata pesa. Pia unapoulizwa kuingiza neno usipoteze muda boya namba inayoendana na mchoro huo.
Lipwa kujiunga
Tunakuletea pia nafasi ya kujiunga na kulipwa, utajiunga na programu zilizotoa hela na hela itakuja kwako. Bofya lipwa kujiunga, angalia kuna tovuti ama program gani zinazotaka ujiunge nazo, tembelea tovuti hizo, jiunge kisha njo hapa na weka ule ujumbe uliotumiwa ulipojiunga, timu ya hisapepe itakagua ujumbe huo na anauani na kulinganisha na tovuti hiyo kisha utajipatia malipo yako. Malipo haya ni baada ya ukaguzi katika tovuti/program yao.
Lipwa Kupitia, Kukagua, Kuthaminisha, Kuchangia maoni ama Kupiga Kura:
Kama kampuni inataka watu waseme kuhusu bidhaa zake, huduma zake ama maoni yao juu ya bidhaa/huduma mpya inayotaka kuja sokoni basi ni hapa ndipo kuna suluhisho la tatizo lao ili kabla ya kuanzaa kampeni na kuzindua huduma/bidhaa wanapata maoni ya wananchi. Pia hapa unaweza kupigia kura jambo lolote au chochote kinachotaka maoni ya jamii (public polling) lakini waendesha kampeni hizi watailipa kampuni ya Hisapepe na Hisapepe itahamishia pesa hiyo kwa mwanachama anayeshiriki. Ingia hisapepe, bofya Lipwa Kupitia. Kisha angalia kila liulizwalo, kama ni kura piga kama ni kuthaminisha basi thamnisha (tumetumia neno RATE 1-5) kura yako ya uthaminisho ni 1 hadi 5, 5 ni bora zaidi na 1 ni ndogo zaidi. Inakuhitaji kujaza maoni yako katika kisanduku kisha unatuma (SUBMIT) na ikipitiwa basi akaunti yako inajipatia pesa. Mara nyingi kiwekwacho hapa kitakuwa na maelezo tosha kwa hiyo usijali utajua tu kama ni kura, maoni, mapitio ama nini. Epuka utani, mzaha na uchafu, hisapepe inachukua kazi za watu makini na tunajinadi tuna wanachama makini, atakayetuma kisicho sawia hakitapitishwa na hatapata ongezeko la salio.
Lipwa Kuchat
Hii si mchezo, badala ya kuchati bure basi unachati hapa, wakati chat inaendelea matangazo yanapita na kila tangazo likipita unaweza kujipatia ela yako, yani ni sehemu ya mawasiliano kulongea ya bure na isitoshe unajipatia pesa juu. Bofya Lipwa Kuchat na anz kuwasiliana na wanachama wenzako, kama una rafiki badala ya kuchat nae kwingine mwambie aje hisapepe kuchat, wakati unachat tangazo likipita usiliache, liofye na utajipatia pesa kadiri ya kiasi kilichowekwa katika tangazo hilo. NB: Chat mpya inakuja, hii ni kwa ajili ya chat ya jumuia (group chat) tupo katika matengenezo ya chat yenye uwezo wa kulonga na mtu chumba chenu (PM), kuwa makini usitoe neno lako la siri unapochat. Hisapepe ama mfanyakazi wake hatakuomba undani wako wowote kupitia chat.
Lipwa Kualika:
Kwa kuwa MTAJI WETU SISI NI WANACHAMA. Kwa sasa tunahitaji watakaojiunga ili tupate wa akutosha na tuanze kurusha matangazo kwa wengi iwezekanavyo. Tumeweka ofa ya muda na ya kudumu. Unajipatia pesa hapo uliyemwalika anapojiunga, na pia ya kudumu ni kwamba unapata kamisheni kila uliyemwalika anapopata pesa hisapepe. Pesa hizi ni bajeti ya kujitangaza (marketing budget) ya Kampuni na ya Hisapepe (tumeona tuwe wakwanza kupeleka ela kwa wanachama wetu)
Kuna njia nyingi za kualika watu
1. Anuani ya Mwaliko (referral link)-hii ni anuani yako wewe popote unapoona inaweza kubofya na kumleta mtu hisapepe.com, akijiunga kupitia kuletwa na anuani hii ni wako umemwalika
Kwa maadhishi-ni kama link tu ukiweka mahali itaonesha hisapepe.com na kama mtu anabofya na kuja basi ni wako.
Kuweka Mabango (banners)
Kama una Tovuti au ukurasa basi weka bango lako la mwaliko na wanaobofya ni wako
Kwa barua pepe (yaani alika kupitia Email)-huenda hii ni bora na nzuri zaidi na hii ina uhakika mkubwa kumfikia mlengwa na si kuishia katika spam/junk/bulk folde. Kumbuka yahoo, gmail, hotmail na wengine hutupa barua pepe fulani katika folda hizo. Hakikisha ujumbe wako ni mfupi na weka anuani yako ya mwaliko, nenda huko katika email yako na “Compose” kisha weka ujumbe wako na tuma kwa marafiki zako ulionao katika anuani zako. Kama hujui cha kuandika hisapepe imeshakuandalia uanaweza kuunakili ujumbe huu katika kisanduku na kuutuma.
Kwa kuingiza anuani za baruapepe na majina
Hii italeta sehemu ya kuweka majina na anuani zao na wote watatumiwa mwaliko. Mwaliko umeshaandikwa kwa ajili yako
MUHIMU SANA
SPAM ni chukizo, hata sisi hisapepe tunachukia, kila mtu anachukia kupokea ujumbe toka kwa mtu asiyemfahamu. Hisapepe haitahusika na mialiko yako zingatia maadili, TUMA MWALIKO KWA RAFIKI NA SI WATU USIOWAJUA. Rafiki akikataa mwaliko usimghasi kwa kuutuma tena na tena.
Hisapepe inashauri njia ya bango (banners) na kama una pa kuliweka tumia njia ya Kualika kupitia email, hii itapunguza kutumia usiowajua
Pia weka banners/mabango panaporuhusiwa. Hisapepe itafunga akaunti za watakaoripotiwa wanaSPAM na watapoteza Salio lao. Tupo makini.
*****Itaendelea*****
Unaweza Kuwasiliana Nasi kama kuna kitu hujaelewa.
|