Walio Hewani: Wanachama 0 | Wageni: 7 |Wanachama Wote: 623 | Tumeshalipa: Tsh 0.00 | Baruapepe ktk Foleni: 0 | Mabango: 12 | Ya Kubofywa: 3

hisapepe.com Masharti Ya Huduma

Kwa kujiunga na kutumia hisapepe.com na programu zake unakubaliana na masharti yote yaliyowekwa katika makubaliano haya. hisapepe.com huenda, kwa wakati wowote, tukaamua kuhariri, kuongeza na/au kufuta sehemu ya makuabaliano haya na kuyaweka hapa bila ya kutaarifu kwanza wanachama wake. Wanachama watafahamishwa mabadiliko kupitia barua pepe zao walizowakilisha wakati wa kujiunga na hisapepe.com Kama mabadiliko yaliyofanyika. Kama mabadiliko hayakubaliki upande wako basi una kila sababu ya kujitoa uanachama. Kuendelea na ushiriki mara baada ya sisi kubadili masharti haya kutamaanisha mbele ya sheria kuwa umekubaliana nayo.
Wajibu wa Wanachama:
Unastahili uwe na umri unaoruhusiwa kushiriki kulingana na sehemu uanyoishi. Kimataifa huwa lazima uwe na walau miaka 13, suala hili la umri tafadhali fautisha sheria za unapoishi. Endapo upo sehemu ambapo ushiriki wa programu hii hauruhusiwi tafadhali usijiunge.

Unakubali ya kwamba utatumia jina na anuani ya barua pepe yako na si ya mtu mwingine wakati wa kujiunga, unakiri kuwa hutatoa taarifa za udanganyifu wa utambulisho. Huruhusiwi kufungua akaunti zaidi ya moja hata kama ni wa kutumia anuani tofauti za barua pepe.
Utatumia anuani ya barua pepe yako na neno lako la siri kuifikia na kuingia katika akaunti yako, ni waajibu wako kuhifadhi kwa siri taarifa za akaunti yako. Wakati wowote unaweza kuhariri na kubadili taarifa zako za akaunti kwa kwenda katika menyu ya "Wasifu Wako".
Ni wewe pekee unawajibika kwa matumizi yoyote na matumizi yote ya akaunti yako hii ikimaanisha hata endapo utakuwa umempatia mtu mwingine na akatumia akaunti yako.

Jaribio lolote la kitapeli, ubadhirifu, au namna nyingine yoyote ya tendo litakaloonekana mbele ya hisapepe.com kuwa ni kinyume na sheria litapelekea akaunti yako kufungwa na huenda sheria ikashika mkondo wake dhidi yako. Udanganyifu au ushawishi wowote wa mwanachama ama mtangazaji/mdhamini kwa dhumuni la kujipatia fedha hautavumilika, akaunti itasitishwa mara moja.
Unalazimika kuendelea kutumia anuani ya barua pepe uliyoiwasilisha ulipojiunga. Unakubali kupokea barua pepe za matangazo kutoka hisapepe.com , idadi ya barua pepe kwa siku moja itategemeana na matangazo yaliyopo kwa siku husika..
Ikitokea ya kwamba anuani ya barua pepe imefungwa au imezuiwa kupokea barua pepe za matangazo toka hisapepe.com , basi akauti yako pia itasitishwa. Hii inamaanisha hata zile barua pepe tutazotuma na kurudushiwa majibu kuwa sanduku lako la barua pepe limejaa hivyo kufanya baruapepe za wadhamini wetu kutokufikia. Mwanachama yeyote atakayetutumia upuuzi au makorokoro ya kutujazia nafasi basi moja kwa moja akaunti yake itasitishwa pia na atakuwa amepoteza mapato yote aliyonayo kama salio la akaunti yake. Wenye anuani za barua pepe walizosifanya zijibu zenyewe (Auto-responses, automatic responders) zitafungiwa pia mara moja. Tafadhali sana, sana zimisha huduma hiyo katika anuani ya barua pepe yako..

Mahusiano ya Pande:
Mkataba wako na sisi ni wa kujitegemea (You and hisapepe.com are independent contractors), na hakuna sehemu katika mkataba huu inayofanya uwe patna, mchangiaji wa mtaji ama gharama, mkurugenzi, wakala, msimamizi wa biashara, mwakilishi wa mauzo/masoko au uhusiano wa mwajiriwa kati ya wewe na hisapepe.com . Unakiri na kuelewa ya kwamba huna mamlaka ya kutoa ama kupokea ofa au kusimama kwa niaba ya hisapepe.com . Huruhusiwi kutoa tamko, popote katika tovuti yako ama kwingineko ambalo linapingana na makubaliano au sehemu ya makubailiano haya. Unawajibika pia kutaarifu vyombo husika juu ya mapato yako ya hapa, kama upo chini ya sheria unapokatwa kodi basi unastahili kutozwa kodi zote husika kadiri unanyojipatia fedha kwa kushiriki programu zetu.

Mipaka ya Madeni :
hisapepe.com haitahusika na upotevu wa faida, fursa za bishara au namna nyingine yoyote ya upotevu isiyo ya moja kwa moja, maalumu, ya kibano, kimatukio, au uharibifu wa kimpelekeo unaoweza kutokea kwa sababu ya makubaliano haya au programu hii, hata kama imeshauriwa juu ya uwezekano wa hasara hizo. Kwa kuongezea, ni kwamba ujumla wa madai ya kulipwa na , hisapepe.com yatakayotokana na makubaliano haya huwezi kuzidi jumla ya ada zote unazostahili kulipwa/kulipa chini ya mkubaliani haya. Matakwa ya kipengele hiki yanategema na usitishwaji wako wa mkataba huu ama kuisha kwa muda wa mkataba huu
Malipo:
Wanachama wataweza kujipatia fedha kwa kupokea barua pepe zenye matangazo na/au kwa kutembelea tovuti za watangazaji/wadhamini. Kwa kujiunga na tovuti zitafutazo wanachama na njia nyingine kadhaa.Wanachama wanaweza pia kujipatia kamisheni kwa kualikwa wanachama wengine wajunge na kuwa chini yao kama waalikwa. Wanachama wanaweza pia kupata kamisheni kama wataweza kuleta mtangazaji/madhamini, watajipatia sehemu ya mpato yanayokusanywa na hisapepe.com .

hisapepe.com italipa mwanachama mara tu afikiapo kiwango kinachoruhusiwa kutoa pesa, kwa sasa ni Tsh 1000/= na itabadilika kadiri ya soko na mapendekezo. Mwanachama akifikiaa kiwango hicho atakuwa na uwezo wa kuomba kulipwa. Kutegemeana na njia ya malipo aliyochagua mwanachama tunahakikisha malipo yamekwenda kwa akaunti mapema iwezekanavyo. Unapojiunga hakikisha unachagua njia ya kulipwa.

Mialiko Jinai/Spam:
Kwa kuwa unalipwa kwa kualikwa wengine unatakiwa kuwa makini. Huruhusiwi kumtumia mtu usiyemfahamu na asiyetaka mwaliko kwa madhumuni ya mumshawishi na kunadi anuani yako ya mialiko. Sheria za intaneti zinakataza hili na ni kosa la jinai. Usifanye hivi kwa mmoja ama makundi ya watu bila kuwafahamu au kutaka. Kinyume na hapo ukiripotiwa tutaisitisha akaunti yako, salio ka akaunti yako na sheria itafuata mkondo wake. Hili ni kosa la jinai.Tunatamka wazi tutashiikiana na vyombo husika kukupata na utashitakiwa. Kwa sasa ikiripotiwa kuwa umetuma barua pepe ya mwaliko usio halali basi kila baruapepe moja huenda ikakugharimu Tsh 5000/=. Tafadhali wajali wenzako wana faragha zao.Kujiunga mara nyingi na programu yetu ni sababu nyingine ya kutufanya tufunge akaunti yako na, watakaogundulika watapoteza mapato yao au kufungiwa kabisa.

Jina Hisapepe

Kwa haraka haraka unaweza sema ni Hisa Za Kielekroniki. Ufinyu wa maneno ya Kiswahili huenda ndio haswa uliosababisha utata. Wamiliki wa programu hii wamehangaika kuitengeneza, kuisimamisha na kuiendesha. Gharama zote juu yao. Leo inaanza na inakuhitaji wewe ushiriki ili iweze kufanya kazi. Kwa tafsiri halisi za hisa au Mwanahisa ulihitaji kuwa umegharamika katika uwekezaji wa hispepe.com. Kwa vile hukushiriki na hutashiriki wewe unakuwa na malipo ya sehemu yako ya utendaji, si sawa na 'hisa' ila neno hisa hapa ni kumaanisha unamiliki gawio la tangazo kadiri ya ushiriki wako. Ibakie kuwa ni hivyo, jione kama ilivyo, pato lako linategemea ushiriki. Faida yake ni kwamba Hutadaiwa hisapepe.com ikidaiwa au kufilisika.

Hii nitafsiri ya Masharti ya Huduma yetu toka lugha ya Kiingereza. Inapotokea mkanganyo kwa sababu ya tafsiri basi itazingatiwa ile ya Kiingereza. Unaweza Kuisoma ya Kiingereza hapa

Hisapepe muuzaji rasmi wa bidhaa na huduma za Scripts-R-Us. Tovuti Scripts-R-Us
Swahili English